Monday, November 28, 2016

MAFUTA YA KITUNGUU SWAUMU NA MATUMIZI YAKE





VITUNGUU SWAUMU hutibu magonjwa mengi sana ikiwa ni pamoja na kushusha presha, kupunguza mafuta mwilini, kutibu ugonjwa wa saratani ‘cancer’, magonjwa ya moyo, hutibu pia kuondoa chunusi.

Leo nitakuelezea mafuta ya kitunguu hiki ni tiba sana ingawa si watu wengi wanayafahamu, yanapatikana maduka yote ya asili ila uwe makini sana kwaababu watengenezaji wamekuwa wengi na yapo chini ya kiwango.

Mafuta haya ukiyatumia ipasavyo yanaouwezo wa kutibu ugonjwa wa mafua, kikohozi kilichoshindikana, yanauwezo wa kutibu fangasi za aina yote na magonjwa mengine mengi.

Kwa wanaopunguza mafuta mwilini
Asubuhi unachukua glasi yako ya maji ya kunywa ambayo umeshayachemsha, yakiwa na uvuguvugu tayari kwa kunywa weka kijiko kimoja kikubwa cha kitunguu swaumu kunywa kila siku asubuhi. Kila mara jaribu kupima uzito utaona matokeo kwani ni tiba nzuri sana mbali na kupunguza mafuta yasiyohitajika mwilini pia yana uwezo wa kupunguza uzito kwa kiasi chake.

Kwa mtu aliyebanwa na mafua
Chukua kitambaa kisafi loweka kwenye mafuta kiasi ni mafuta yenye harufu kali ambayo unaweza usiivumilie lakini kitiba yanatibu kwa haraka sana.
Kama una uwezo wa kuweka kwenye maji yaliyochemka na kujifukiza, husaidia kufungua pua na kukutibu kikohozi ambacho huletwa na mafua.

Kwa akina mama wanaotaka kurudisha umwari wao
Kwa wale akina mama ambao wamekuwa na tabia ya kutaka kurudisha umwari wao, hasa wale waliozaa na wale ambao wanahisi hawako sawa mafuta haya yanasaidia iwapo utapaka hasa wakati wa kulala.

Kwa kutibu fangasi
Fangasi wapo wa aina nyingi hapa niongelee wa miguuni na wa sehemu za siri.
Mafuta haya yanatibu kwa asilimia kubwa tatizo la fangasi kama unao wa miguuni, chukua mafuta haya yapashe kidogo yaache yapoe, osha miguu yako ikaushe mpaka katikati ya vidole kisha chukua mafuta ya kitunguu swaumu paka mpaka utakapoona umepona.
Kwa walio na fangasi wa sehemu za siri hasa akina mama, chukua maji ya vuguvugu, weka mafuta hayo kiasi cha vijiko viwili kwenye maji nawa na maji hayo sehemu za siri unaweza kufanya hivyo mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jion.

Maumivu ya sikio
Kama unasumbuliwa na sikio mafuta haya ni tiba nzuri, chukua mafuta yapashe yaache yapoe kabisa, kisha dondoshea tone moja kwa mtoto na kwa wakubwa matone 2-3, kama huna mafuta haya unaweza kuchukua mafuta ya mzaituni ukayapasha kidogo nayo uache yapoe kisha changanya na vipande viwili vya vitunguu swaumu udondoshee kama mafuta hayo, fanya hivyo mpaka utakapopona

Kumbuka
Kuwa makini na mafuta yanayouzwa kiholela huweza kukuletea matatizo hakikisha yamethibitishwa na TBS.    PIA
Mafuta haya ya KITUNGUU SWAUMU ukiwa unayatumia sehemu za siri usichanganye na mafuta mengine yeyote. 
NARUDIA USICHANGANYE NA MAFUTA YEYOTE UKENI  HADI UMALIZE TIBA.

Ukitaka mafuta haya nipigie ni  10,000/=
#0657904346


Tuesday, November 1, 2016

Mask ya ndizi na asali kwa ajili ya ngozi zenye mafuta







 



Namna ya kutengeneza mask ya ndizi na asali kwa ajili ya ngozi zenye mafuta na kutoka chunusi.

Vinavyohitajika
• Ndizi moja iliyoiva vyema.
• Asali kijiko kimoja cha chakula.

 • Limau, ndimu au chungwa moja
.


Namna ya kutengenza:
1. Menya ndizi na uiponde vizuri, kisha changanya katika kibakuli safi pamoja na asali.
2. Kamua limau, ndimu au chungwa, toa kokwa na maji yake changanya kwenye mchanganyiko wa ndizi na asali.
3. Chanyanya vizuri hadi upate mchanganyiko sawia.
4. Paka mchanganyiko huo usoni na shingoni bila kuweka machoni.
5. Wacha kwa muda wa dakika 15 na osha kwa maji ya uvuguvugu.


 Maoni yako ni muhimu sana ukituachia. 
Kama unalolote ungependa kushare nasi nitumie tuttyrahma@gmail.com