Dawa mbadala ya vidonda vya tumbo
1. KabejiKabeji ni moja ya dawa bora za asili zinazoweza kutibu vodonda vya tumbo. Kabeji inayo ‘lactic acid’ na husaidia kutengeneza amino asidi ambayo huhamasisha utiririkaji wa damu kwenda kwenye kuta za tumbo jambo linalosaidia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo na hatimaye kutibu vidonda vya tumbo.
Kabeji pia ina kiasi kingi cha vitamini C ambayo imethibitika kuwa na faida kubwa kwa watu wenye vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na maambukizi ya bakteria aitwaye ‘H. pylori. Pia majaribio yamethibitisha kuwa juisi ya karoti freshi inayo vitamini U mhimu kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo.
- Kata kabeji nzima mara mbili na uchukuwe nusu yake, chukuwa karoti mbili na ukatekate vipande vidogo vidogo na utumbukize vyote kabeji na karoti kwenye blenda na uvisage ili kupata juisi yake.
- Kunywa kikombe kimoja cha juisi hii kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni na kikombe kimoja kabla hujaingia kulala.
- Rudia zoezi hili kila siku kwa wiki kadhaa na hakikisha unatumia juisi freshi pekee na siyo ukanunue juisi ya kabeji au karoti ya dukani.
2. Ndizi
Ndizi zilizoiva na hata ambazo hazijaiva zote ni nzuri kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo. Kuna aina maalumu ya muunganiko wa vimeng’enya vilivyomo kwenye ndizi ambavyo huzuia kuongezeka au kuzaliana kwa bakteria wa vidonda vya tumbo ‘H. Pylori’.
Ndizi pia huulinda mfumo wa kuta za tumbo kwa kuiondoa asidi iliyozidi tumboni na hivyo kusaidia kuuondoa uvimbe au vidonda tumboni na pia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo.
- Ili kutibu vidonda vya tumbo, kula walau ndizi zilizoiva 3 kwa siku.
- Au menya ndizi 2 au 3 na uzikate katika vipande vidogo vyembamba (slices) na uanike juani mpaka zikauke kabisa. Kisha saga vipande hivyo ili kupata unga na uchanganye vijiko vikubwa viwili vya unga huu na kijiko kikubwa kimoja cha asali na ulambe mchanganyiko huu mara 3 kwa siku kwa wiki 2 hivi.
3. Nazi
Nazi ni nzuri sana katika kutibu vidonda vya tumbo sababu ya sifa yake na uwezo wa kuua bakteria. Nazi huziua bakteria zinazosababisha vidonda vya tumbo. Pia tui la nazi na maji ya nazi (dafu) vyote vina sifa na uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo.
- Kunywa vikombe kadhaa vya tui freshi la nazi au maji ya nazi kila siku. Pia unaweza kuitafuana nazi yenyewe mara kwa mara. Fuatisha mlolongo huu walau kwa wiki 2 ili kupata matokeo chanya.
- Au kunywa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya asili ya nazi asubuhi kabisa na kingine usiku kwa wiki 2 hivi.
4. Uwatu
Uwatu unajulikana sana kwa uwezo wake wa kutibu maradhi mengi mwilini. Unaweza pia kuutumia katika kutibu vidonda vya tumbo. Kwakuwa uwatu inayo gundi maalumu au ulimbo ambayo huulinda ukuta wa tumbo kwa kuufunga au kuufunika kama utando na hivyo kurahisisha hatua za kutibu vidonda vya tumbo.
- Chemsha mbegu za uwatu kijiko kidogo cha chai ndani ya vikombe viwili vya maji, chuja na uongeze asali kidogo na unywe kwa pamoja kutwa mara 2 kwa wiki 2 au zaidi.
- Unaweza pia kutumia kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa mbegu za uwatu ukichanganya kwenye kikombe cha maziwa ya moto.
- Au unaweza kuchemsha kikombe kimoja cha majani freshi ya uwatu, ongeza asali kidogo na unywe mara 2 kwa siku kwa wiki 2 au zaidi.
- Ingawa maziwa hayashauriwi sana kutumika kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo, hivyo unaweza kutumia maji ya uvuguvugu badala ya maziwa kama vidonda vyako vimeshakuwa sugu sana au ikiwa unahitaji upate nafuu ya haraka na hatimaye kupona.
5. Asali
Asali mbichi, ile nzuri kabisa ambayo haijachakachuliwa inao uwezo mkubwa katika kutibu vidonda vya tumbo. Kama ujuavyo asali ni dawa karibu kwa kila ugonjwa. Kuna kimeng’enya kilichomo kwenye asali kijulikanacho kama ‘glucose oxidase’ ambacho huizalisha ‘hydrogen peroxide’ ambayo yenyewe inayo uwezo wa kuuwa bakteria wabaya mwilini ambao husababisha vidonda vya tumbo. Pia hii ‘glucose oxidase’ huulainisha ukuta wa tumbo na kupunguza muwako au vidonda tumboni.
Lamba vijiko vikubwa viwili kutwa mara tatu au vijiko vikubwa vitatu kutwa mara mbili. Itasaidia kusafisha tumbo, itaimarisha ukuta wa tumbo na kuzuia na kutibu vidonda vya tumbo. Fanya hivi kwa wiki 3 hadi 4. Hakikisha unapata asali mbichi salama ambayo haijachakachuliwa.
6. Kitunguu Swaumu
Kitunguu swaumu pia husaidia kutibu vidonda vya tumbo. Watafiti katika kituo cha utafiti wa kansa cha Fred Hutchinson Cancer Research Center in Seattle waligundua kuwa uwezo ambao kitunguu swaumu unacho katika kudhibiti na kuua bakteria mbalimbali mwilini unaweza kudhiti pia bakteria anayesababisha vidonda vya tumbo ajulikanaye kama Helicobacter Pylori (H. pylori).
Chukuwa punje 6 hadi 10 za kitunguu swaumu, menya na ukate vipande vidogo vidogo kisha umeze pamoja na maji vikombe viwili kutwa mara 2 kwa wiki 2 au 3.
7. Mkaa wa kifuu cha nazi
Mkaa pia hutibu vidonda vya tumbo hasa mkaa utokanao na vifuu vya nazi. Chukua vifuu vya nazi vitano au kumi vilivyokauka, viweke juu ya jiko la mkaa au popote na uvichome moto, mwishoni chukua mkaa wake usage kupata unga, kisha chota kijiko kikubwa kimoja na uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji changanya vizuri na unywe kutwa mara 3 kwa wiki 2 au 3.
8. Unga wa majani ya Mlonge
Mlonge ni mti mhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali. Mlonge una kiasi kingi cha vitamin C, Madini ya chuma, protini, Vitamini A na potasiamu.
Ongeza kijiko kimoja cha chakula kwenye bakuli ya mboga unapokula chakula cha mchana na jioni. Unaweza pia kunywa unga huu wa mlonge pamoja na juisi yoyote uliyotengeneza mwenyewe nyumbani au unaweza kuuchanganya kwenye chakula kama vile wali na hivyo ukajiongezea kinga zako dhidi ya vidonda vya tumbo. Tumia kwa wiki 3 hadi 4.
Chagua dawa mbili au tatu kati ya hizi na uzitumie kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri zaidi. Na kwa hapa napendekeza zaidi dawa namba tatu, tano, sita na nane. Usisahahu pia kunywa maji ya kutosha kila siku.
Kwa mahitaji ya dawa hizi na maswali na ushauri zaidi: +255 657904346
Jiunge na ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa => facebook