Dry
hands inaweza kuwa imesababishwa na vitu vingi, either baridi au hata kuwa
hau-moisturize mikono vizuri ndio maana mikono yako inakua inakauka na hata
kupasuka, unatokewa cracks.
1.Tengeneza paste nzito kwa kutumia 1/2
parachichi, kijiko 1 cha olive oil na 1 cha apple cider vinegar. Changanya
vizuri upate mchanganyiko mzito. Paka kwenye mikono yako na ukae nayo kwa
dakika 15 then nawa kwa maji ya uvuguvugu..utaona mikono imekuwa milaini, fanya
hivi kila siku ili upate results nzuri.
2.Chukua apple cider vinegar changanya na maji
kwenye bakuli, kisha loweka mikono yako humo kwa muda. Toa na uache mikono
ikauke yenyewe. Apple cider vinegar inasaidia kuondoa maumivu kutokana na
mikono kukauka sana.
3.Chukua kiini cha yai, juice ya ndimu na
kijiko 1 cha olive oil. Changaya vizuri katika bakuli kisha paka kwenye mikono
yako na kaa nayo kwa dakika 15. Nawa mikono na maji ya uvuguvugu kisha paka
moisturizer.
4.Tengeneza hand cream yako mwenyewe kwa
kutumia rose water, juice ya ndimu na glycerine. Changanya vyote hivi kupata
moisturizer kwa ajili ya mikono yako.
5.Tengeneza juice ya
matango na uichanganye na glycerine. Tumia kila siku usiku itakusaidia
kulainisha ngozi yako.