Monday, November 28, 2016

MAFUTA YA KITUNGUU SWAUMU NA MATUMIZI YAKE





VITUNGUU SWAUMU hutibu magonjwa mengi sana ikiwa ni pamoja na kushusha presha, kupunguza mafuta mwilini, kutibu ugonjwa wa saratani ‘cancer’, magonjwa ya moyo, hutibu pia kuondoa chunusi.

Leo nitakuelezea mafuta ya kitunguu hiki ni tiba sana ingawa si watu wengi wanayafahamu, yanapatikana maduka yote ya asili ila uwe makini sana kwaababu watengenezaji wamekuwa wengi na yapo chini ya kiwango.

Mafuta haya ukiyatumia ipasavyo yanaouwezo wa kutibu ugonjwa wa mafua, kikohozi kilichoshindikana, yanauwezo wa kutibu fangasi za aina yote na magonjwa mengine mengi.

Kwa wanaopunguza mafuta mwilini
Asubuhi unachukua glasi yako ya maji ya kunywa ambayo umeshayachemsha, yakiwa na uvuguvugu tayari kwa kunywa weka kijiko kimoja kikubwa cha kitunguu swaumu kunywa kila siku asubuhi. Kila mara jaribu kupima uzito utaona matokeo kwani ni tiba nzuri sana mbali na kupunguza mafuta yasiyohitajika mwilini pia yana uwezo wa kupunguza uzito kwa kiasi chake.

Kwa mtu aliyebanwa na mafua
Chukua kitambaa kisafi loweka kwenye mafuta kiasi ni mafuta yenye harufu kali ambayo unaweza usiivumilie lakini kitiba yanatibu kwa haraka sana.
Kama una uwezo wa kuweka kwenye maji yaliyochemka na kujifukiza, husaidia kufungua pua na kukutibu kikohozi ambacho huletwa na mafua.

Kwa akina mama wanaotaka kurudisha umwari wao
Kwa wale akina mama ambao wamekuwa na tabia ya kutaka kurudisha umwari wao, hasa wale waliozaa na wale ambao wanahisi hawako sawa mafuta haya yanasaidia iwapo utapaka hasa wakati wa kulala.

Kwa kutibu fangasi
Fangasi wapo wa aina nyingi hapa niongelee wa miguuni na wa sehemu za siri.
Mafuta haya yanatibu kwa asilimia kubwa tatizo la fangasi kama unao wa miguuni, chukua mafuta haya yapashe kidogo yaache yapoe, osha miguu yako ikaushe mpaka katikati ya vidole kisha chukua mafuta ya kitunguu swaumu paka mpaka utakapoona umepona.
Kwa walio na fangasi wa sehemu za siri hasa akina mama, chukua maji ya vuguvugu, weka mafuta hayo kiasi cha vijiko viwili kwenye maji nawa na maji hayo sehemu za siri unaweza kufanya hivyo mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jion.

Maumivu ya sikio
Kama unasumbuliwa na sikio mafuta haya ni tiba nzuri, chukua mafuta yapashe yaache yapoe kabisa, kisha dondoshea tone moja kwa mtoto na kwa wakubwa matone 2-3, kama huna mafuta haya unaweza kuchukua mafuta ya mzaituni ukayapasha kidogo nayo uache yapoe kisha changanya na vipande viwili vya vitunguu swaumu udondoshee kama mafuta hayo, fanya hivyo mpaka utakapopona

Kumbuka
Kuwa makini na mafuta yanayouzwa kiholela huweza kukuletea matatizo hakikisha yamethibitishwa na TBS.    PIA
Mafuta haya ya KITUNGUU SWAUMU ukiwa unayatumia sehemu za siri usichanganye na mafuta mengine yeyote. 
NARUDIA USICHANGANYE NA MAFUTA YEYOTE UKENI  HADI UMALIZE TIBA.

Ukitaka mafuta haya nipigie ni  10,000/=
#0657904346


Tuesday, November 1, 2016

Mask ya ndizi na asali kwa ajili ya ngozi zenye mafuta







 



Namna ya kutengeneza mask ya ndizi na asali kwa ajili ya ngozi zenye mafuta na kutoka chunusi.

Vinavyohitajika
• Ndizi moja iliyoiva vyema.
• Asali kijiko kimoja cha chakula.

 • Limau, ndimu au chungwa moja
.


Namna ya kutengenza:
1. Menya ndizi na uiponde vizuri, kisha changanya katika kibakuli safi pamoja na asali.
2. Kamua limau, ndimu au chungwa, toa kokwa na maji yake changanya kwenye mchanganyiko wa ndizi na asali.
3. Chanyanya vizuri hadi upate mchanganyiko sawia.
4. Paka mchanganyiko huo usoni na shingoni bila kuweka machoni.
5. Wacha kwa muda wa dakika 15 na osha kwa maji ya uvuguvugu.


 Maoni yako ni muhimu sana ukituachia. 
Kama unalolote ungependa kushare nasi nitumie tuttyrahma@gmail.com

Wednesday, October 12, 2016

Dawa mbadala ya vidonda vya tumbo



                                           vidonda vya tumbo.
 

Dawa mbadala ya vidonda vya tumbo

1. Kabeji
Kabeji
Kabeji
Kabeji ni moja ya dawa bora za asili zinazoweza kutibu vodonda vya tumbo. Kabeji inayo ‘lactic acid’ na husaidia kutengeneza amino asidi ambayo huhamasisha utiririkaji wa damu kwenda kwenye kuta za tumbo jambo linalosaidia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo na hatimaye kutibu vidonda vya tumbo.
Kabeji pia ina kiasi kingi cha vitamini C ambayo imethibitika kuwa na faida kubwa kwa watu wenye vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na maambukizi ya bakteria aitwaye ‘H. pylori. Pia majaribio yamethibitisha kuwa juisi ya karoti freshi inayo vitamini U mhimu kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo.
  1. Kata kabeji nzima mara mbili na uchukuwe nusu yake, chukuwa karoti mbili na ukatekate vipande vidogo vidogo na utumbukize vyote kabeji na karoti kwenye blenda na uvisage ili kupata juisi yake.
  2. Kunywa kikombe kimoja cha juisi hii kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni na kikombe kimoja kabla hujaingia kulala.
  3. Rudia zoezi hili kila siku kwa wiki kadhaa na hakikisha unatumia juisi freshi pekee na siyo ukanunue juisi ya kabeji au karoti ya dukani.

2. Ndizi
Ndizi
Ndizi
Ndizi zilizoiva na hata ambazo hazijaiva zote ni nzuri kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo. Kuna aina maalumu ya muunganiko wa vimeng’enya vilivyomo kwenye ndizi ambavyo huzuia kuongezeka au kuzaliana kwa bakteria wa vidonda vya tumbo ‘H. Pylori’.
Ndizi pia huulinda mfumo wa kuta za tumbo kwa kuiondoa asidi iliyozidi tumboni na hivyo kusaidia kuuondoa uvimbe au vidonda tumboni na pia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo.
  • Ili kutibu vidonda vya tumbo, kula walau ndizi zilizoiva 3 kwa siku.
  • Au menya ndizi 2 au 3 na uzikate katika vipande vidogo vyembamba (slices) na uanike juani mpaka zikauke kabisa. Kisha saga vipande hivyo ili kupata unga na uchanganye vijiko vikubwa viwili vya unga huu na kijiko kikubwa kimoja cha asali na ulambe mchanganyiko huu mara 3 kwa siku kwa wiki 2 hivi.

3. Nazi
Nazi ni nzuri sana katika kutibu vidonda vya tumbo sababu ya sifa yake na uwezo wa kuua bakteria. Nazi huziua bakteria zinazosababisha vidonda vya tumbo. Pia tui la nazi na maji ya nazi (dafu) vyote vina sifa na uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo.
  • Kunywa vikombe kadhaa vya tui freshi la nazi au maji ya nazi kila siku. Pia unaweza kuitafuana nazi yenyewe mara kwa mara. Fuatisha mlolongo huu walau kwa wiki 2 ili kupata matokeo chanya.
  • Au kunywa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya asili ya nazi asubuhi kabisa na kingine usiku kwa wiki 2 hivi.


4. Uwatu
Uwatu
Uwatu
Uwatu unajulikana sana kwa uwezo wake wa kutibu maradhi mengi mwilini. Unaweza pia kuutumia katika kutibu vidonda vya tumbo. Kwakuwa uwatu inayo gundi maalumu au ulimbo ambayo huulinda ukuta wa tumbo kwa kuufunga au kuufunika kama utando na hivyo kurahisisha hatua za kutibu vidonda vya tumbo.
  • Chemsha mbegu za uwatu kijiko kidogo cha chai ndani ya vikombe viwili vya maji, chuja na uongeze asali kidogo na unywe kwa pamoja kutwa mara 2 kwa wiki 2 au zaidi.
  • Unaweza pia kutumia kijiko kidogo kimoja cha chai cha unga wa mbegu za uwatu ukichanganya kwenye kikombe cha maziwa ya moto.
  • Au unaweza kuchemsha kikombe kimoja cha majani freshi ya uwatu, ongeza asali kidogo na unywe mara 2 kwa siku kwa wiki 2 au zaidi.
  • Ingawa maziwa hayashauriwi sana kutumika kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo, hivyo unaweza kutumia maji ya uvuguvugu badala ya maziwa kama vidonda vyako vimeshakuwa sugu sana au ikiwa unahitaji upate nafuu ya haraka na hatimaye kupona.

5. Asali
dawa mbadala zinazotibu pumu
Asali
Asali mbichi, ile nzuri kabisa ambayo haijachakachuliwa inao uwezo mkubwa katika kutibu vidonda vya tumbo. Kama ujuavyo asali ni dawa karibu kwa kila ugonjwa. Kuna kimeng’enya kilichomo kwenye asali kijulikanacho kama ‘glucose oxidase’ ambacho huizalisha ‘hydrogen peroxide’ ambayo yenyewe inayo uwezo wa kuuwa bakteria wabaya mwilini ambao husababisha vidonda vya tumbo. Pia hii ‘glucose oxidase’ huulainisha ukuta wa tumbo na kupunguza muwako au vidonda tumboni.
Lamba vijiko vikubwa viwili kutwa mara tatu au vijiko vikubwa vitatu kutwa mara mbili. Itasaidia kusafisha tumbo, itaimarisha ukuta wa tumbo na kuzuia na kutibu vidonda vya tumbo. Fanya hivi kwa wiki 3 hadi 4. Hakikisha unapata asali mbichi salama ambayo haijachakachuliwa.

6. Kitunguu Swaumu
Kitunguu swaumu
Kitunguu swaumu
Kitunguu swaumu pia husaidia kutibu vidonda vya tumbo. Watafiti katika kituo cha utafiti wa kansa cha Fred Hutchinson Cancer Research Center in Seattle waligundua kuwa uwezo ambao kitunguu swaumu unacho katika kudhibiti na kuua bakteria mbalimbali mwilini unaweza kudhiti pia bakteria anayesababisha vidonda vya tumbo ajulikanaye kama Helicobacter Pylori (H. pylori).
Chukuwa punje 6 hadi 10 za kitunguu swaumu, menya na ukate vipande vidogo vidogo kisha umeze pamoja na maji vikombe viwili kutwa mara 2 kwa wiki 2 au 3.

7. Mkaa wa kifuu cha nazi
Vifuu vya Nazi
Vifuu vya Nazi
Mkaa pia hutibu vidonda vya tumbo hasa mkaa utokanao na vifuu vya nazi. Chukua vifuu vya nazi vitano au kumi vilivyokauka, viweke juu ya jiko la mkaa au popote na uvichome moto, mwishoni chukua mkaa wake usage kupata unga, kisha chota kijiko kikubwa kimoja na uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji changanya vizuri na unywe kutwa mara 3 kwa wiki 2 au 3.

8. Unga wa majani ya Mlonge
mlonge
Mlonge ni mti mhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali. Mlonge una kiasi kingi cha vitamin C, Madini ya chuma, protini, Vitamini A na potasiamu.
Ongeza kijiko kimoja cha chakula kwenye bakuli ya mboga unapokula chakula cha mchana na jioni. Unaweza pia kunywa unga huu wa mlonge pamoja na juisi yoyote uliyotengeneza mwenyewe nyumbani au unaweza kuuchanganya kwenye chakula kama vile wali na hivyo ukajiongezea kinga zako dhidi ya vidonda vya tumbo. Tumia kwa wiki 3 hadi 4.

Chagua dawa mbili au tatu kati ya hizi na uzitumie kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri zaidi. Na kwa hapa napendekeza zaidi dawa namba tatu, tano, sita na nane. Usisahahu pia kunywa maji ya kutosha kila siku.



Kwa mahitaji ya dawa hizi na  maswali na ushauri zaidi: +255 657904346
Jiunge na ukurasa wangu wa facebook kwa kubonyeza hapa => facebook

Monday, October 10, 2016

HII NDIO TIBA ASILI YA UGONJWA WA BAWASIRI

 

Bawasiri katika mzunguko wa tundu la njia ya haja kubwa

Ugonjwa huu wa bawasiri ni ugonjwa unaotokana na kuvimba kwa mishipa ya damu katika mfereji wa njia ya haja kubwa. Ugonjwa huu katika jamii hufahamika kwa majina tofauti tofauti hutegemea kabila na mahali. 

              Ugonjwa huu umekua ni ugonjwa hatari kutokana na tabia za wagonjwa kuficha kutokana na aibu ya tatizo lenyewe lilipo au kuhofia jamii kumtazama tofauti kwa sababu jamii nyingi hasa za afrika mashariki zinaamini kuwa ugonjwa huu ni mkosi mkubwa.
              Kuna aina kuu mbili za bawasiri 1; Bawasiri ya nje 2; Bawasiri ya ndani. 
Bawasiri hii ya ndani ndio bawasiri mbaya kabisa kwa sababu ni vigumu mgonjwa kujitambua kua anatatizo na hii inatokana na tabia ya bawasiri yandani kutokua na maumivu wakati inaanza.
SABABU ZINAZOPELEKEA MTU KUPATA BAWASIRI
             
 Ugonjwa huu wa bawasiri husababishwa na mambo yafuatayo;

(1) Tabia ya kuketi sehemu moja kwa muda mrefu mfano; madereva
(2) Tatizo sugu la kuharisha
3) Ujauzito
(4) Uzito wa mwili kupita kiasi
(5) Kufanya ngono kupitia tundu la haja kubwa  (kulawitiwa)
(6) Kupata haja kubwa ngumu
(7) Kua na mgandamizo mkubwa tumboni.
                     


ATHARI ZA BAWASIRI
* Upungufu wa damu mwilini
* Kutokwa na kinyesi bila kijitambua 
* kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa
* kupungukia nguvu za kiume (kwa wanaume)
* kupungukiwa na uwezo wa kufanya kazi kutokana na maumivu
* Kupata tatizo la kisaikolojia 

NJIA ZA KUJIKINGA DHIDI YA BAWASIRI
* Kula mboga za majani na nafaka zisizo kobolewa kwa wingi 
* kunywa maji mengi lita sita hadi kumi na mbili kwa siku
* Acha kufanya ngono kwa kutumia tundu la haja kubwa (kulawitiwa)
* Punguza kukaa chooni kwa muda mrefu, kunaweza kuongeza shinikizo katika njia ya haja kubwa.


              TIBA YA KISASA   (KISAYANSI)
Kama tulivyo elezea ugonjwa huu ni kuvimba kwa mishipa ya damu katika mfereji wa njia ya haja kubwa sasa njia zifuatazo hutumika kutibu ugonjwa huu.

1*  Mishipa ya damu kufungwa Rubber band
2*  Kuweka kemikali kwa njia ya sindano
3*  Upasuaji
             

TIBA ASILIA 
Zifuatazo ni njia za kutibu  ugonjwa huo wa bawasiri kwa dawa za asili;
         
         1;  Mizizi ya mti wa Mkomamanga ya kutosha kuanzia ujazo wa robo kilo na kuendelea ichemshwe na lita moja na nusu ya maji na vijiko vitatu vya Ubani Makka. hakikisha unakunywa dawa hiyo mara tatu kwa kutwa kwa muda wa siku saba hadi kumi na nne

       2.     Juisi fresh ya jani lililokamaa la Aloe Vera ni dawa nzuri na huondosha bawasiri
       
      3.   (i) Asali nusu lita 
            (ii) Unga wa Tangawizi vijiko vitatu
           (iii) Unga wa figili vijiko vitatu
           (iv) Unga wa kitunguu swaumu vijiko vitatu
vitu vyote vichanganywe vizuri mgonjwa awe anakula kijiko kimoja cha mchanganyiko huo mara tatu kwa kutwa kwa muda wa siku 21. 
               swali , maoni au ushauri wako ni muhimu
shida binafsi : tuttyrahma@gmail.com
+255 657904346

JIFUNZE JINSI YA KUTENGENEZA DAWA YA KUONGEZA UUME


 

UUME
UUME WA WASTANI
Watu wengi wamekua wakihangaika kutafuta dawa ya kuongeza Uume bila mafanikio pia kuna watu ambao wamepata madhara maada ya kutumia dawa za kuongeza Uume na hii inatokana na matumizi ya dawa za kemikali
Pia kuna wengine wamekata tamaa na kudhani kua hakuna dawa ya kuongeza Uume  ila ni udanganyifu tu. ukweli ni kwamba dawa zipo tatizo ni kuzijua tu
Ili kutengeneza dawa ya kukuza Uume fuata hatua zifuatazo
Tafuta dawa zifutazo.
1. Unga wa Pilipili mtama Nyeupe (Filfil Abiadh) kijiko kimoja
2.Pilipili Baridi vijiko viwili
3.Kibiriti upele kijiko kimoja
Changanya vizuri na asali mbichi ya nyuki.
Matumizi
1.Osha uume wako kwa maji vuguvugu  dakika 3 mpaka 5
2.Uchue uume wako kwa mchanganyiko huo wa asali kwa dakika 7 
3. Fanya zoezi hilo kila siku kwa matokeo mazuri na haraka zaidi.
4.Endelea na zoezi mpaka itakapofikia saizi uitakayo.
UUME MKUBWA
UUME MKUBWA

NB; Dawa hii ni ya asili na haina madhara yoyote.
Dawa hii haina masharti yoyote wakati utumiapo. ni dawa ya asili na imemsaidia kila aliotumia kwa usahihi.

Thursday, August 18, 2016

5 TIPS ZA KUPATA MIKONO LAINI.







Dry hands inaweza kuwa imesababishwa na vitu vingi, either baridi au hata kuwa hau-moisturize mikono vizuri ndio maana mikono yako inakua inakauka na hata kupasuka, unatokewa cracks.


Ni ngumu sana kupata moisturizer ambayo itapenda ngozi yako na kukusaidia ngozi iwe laini, sio lazima kutumia hela nyingi kununua cream ambayo itaondoa hilo tatizo, unaweza pia kutumia nutural remedies/njia asili kima ifuatayo..

1.Tengeneza paste nzito kwa kutumia 1/2 parachichi, kijiko 1 cha olive oil na 1 cha apple cider vinegar. Changanya vizuri upate mchanganyiko mzito. Paka kwenye mikono yako na ukae nayo kwa dakika 15 then nawa kwa maji ya uvuguvugu..utaona mikono imekuwa milaini, fanya hivi kila siku ili upate results nzuri.



2.Chukua apple cider vinegar changanya na maji kwenye bakuli, kisha loweka mikono yako humo kwa muda. Toa na uache mikono ikauke yenyewe. Apple cider vinegar inasaidia kuondoa maumivu kutokana na mikono kukauka sana.



3.Chukua kiini cha yai, juice ya ndimu na kijiko 1 cha olive oil. Changaya vizuri katika bakuli kisha paka kwenye mikono yako na kaa nayo kwa dakika 15. Nawa mikono na maji ya uvuguvugu kisha paka moisturizer.






4.Tengeneza hand cream yako mwenyewe kwa kutumia rose water, juice ya ndimu na glycerine. Changanya vyote hivi kupata moisturizer kwa ajili ya mikono yako.


5.Tengeneza juice ya matango na uichanganye na glycerine. Tumia kila siku usiku itakusaidia kulainisha ngozi yako.